Mahitaji
Tambi
Sukari
Mafuta ya kupikia
Maji
Hiliki
Matayarisho
- Weka tambi katika sufuria ya saizi ya kati na kama tambi ni ndefu unaweza ukazikata mara tatu au mbili ili ziendelee kuwa ndefu kidogo.
- Weka maji katika sufuria yenye tambi kisha bandika jikoni zichemke kwa dakika 10 mpaka 15 huku ukihakikisha haziivi sana
- Kisha ipua chuja kwenye chujio toa maji yote
- Weka mafuta kwenye sufuria
- Weka tambi kisha weka sukari na hiliki
- Endelea kugeuza na kisha ipua.
- Tambi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa zikiwa nzuri za kuvutia.
No comments:
Post a Comment