Pilau ni chakula kinacholiwa na wengi katika hafla mbalimbali na watu wengi husema sherehe bila pilau basi bado haijakamilika. Tuangalie pishi la pilau
Mahitaji
Kitunguu maji
Vitunguu swaumu
Viungo vya pilau
Chumvi
Maji
Mafuta ya kupikia
Mchele
Maandalizi
- Unakaanga kitunguu maji na kitunguu swaumu kwa mafuta kiasi yani kama kijiko kimoja cha kulia chakula
- Unaweka viungo vya pilau vilivyosagwa kisha unavikaanga
- Weka mchele kisha geuza na weka maji kiasi kulingana na mchele kisha weka chumvi kiasi
- Acha vitokote ili viweze kuiva vizuri
- Maji yakikauka angalia kama pilau limeiva vizuri kisha palia juu na chini kama unapikia mkaa na kama ni gesi angalia kama umeiva vzr na upunguze moto kabisa ili ukauke vizuri.
- Pilau lako litakuwa tayari baada ya kuiva vizuri.
No comments:
Post a Comment