Mahitaji
Ndizi mzuzu
Chumvi
Nazi
Binzari nyembamba
Kuku robo
Nyanya
Kitunguu maji
Kitunguu swaumu
Karoti
Hoho
Maandalizi
- Menya ndizi zako vizuri kisha weka kwenye maji ili zisiwe nyeusi.
- Weka ndizi zako kwenye sufuria safi kisha weka Nazi tui la pili jepesi ili zichemke kwa Nazi
- Kisha weka vitunguu swaumu na vitunguu maji
- Baada ya hapo weka nyanya, karoti, na hoho
- Kisha weka vipande vya kuku vilivyochemshwa vizuri ilivichemke tena na ndizi
- Weka tui la pili zito la Nazi na koroga mpaka lichemke vizuri
- Weka chumvi na binzari nyembamba kidogo sana
- Ipua ndizi kwaajili ya kuliwa
No comments:
Post a Comment