Mahitaji
Vitunguu maji 3
Hoho 1
Karoti 1
Nyanya 4
Chumvi
Ndimu 1
Tango 1
Maandalizi
- Osha viungo vyote kwa chumvi kiasi na maji ya uvuguvugu
- Katakata nyanya kwa namna ya duara kisha weka kwenye bakuri
- Kisha katakata karoti na tango duara
- Katakata hoho kwa wima yani ziwe kama namba moja kisha weka vyote kwenye bakuri ya nyanya
- Katakata vitunguu maji weka kwenye bakuri tofauti kisha weka chumvi na vifinyange kwa chumvi ilikupunguza makali ya vitunguu maji.
- Kisha osha vizuri kwa maji na kamua ili kuhakikisha chumvi haipo kwenye vitunguu tena na maji hayapo
- Weka vitunguu kwenye bakuri yenye vitu vyote na kisha changanya vizuri kwa kutumia kijiko.
- Baada ya hapo weka chumvi kidogo na maji ya ndimu ambayo umeikamua
- Kisha changanya na kachumbari yako itakuwa tayari kuliwa
No comments:
Post a Comment