Mahitaji
Maharage
Vitunguu swaumu
Vitunguu maji
Karoti
Pilipili hoho
Chumvi
Nazi
Tangawizi
Maandalizi
- Chambua, osha na kisha chemsha maharage yako mpaka yaive vizuri hakikisha maji ya kwanza yanakuwa mengi ili maharage yasiungue.
- Yakishaiva ipua na chukua sufuria ya kukaangia na weka mafuta kidogo sana
- Weka kitunguu maji ulichokatakata na baadae kitunguu swaumu na tangawizi
- Weka maharage na kisha weka nazi tui la pili na koroga mpaka lichemke vizuri
- Kisha weka tui la kwanza zito nalo lichemke vizuri ndo uache kukoroga
- Weka hoho na karoti baada ya tui la kwanza zito kuchemka na uache vichemke kidogo kisha weka na chumvi kidogo kutokana na wingi wa maharage yako.
- Baada ya hapo maharage yako yatakuwa yameiva vizuri sana.
No comments:
Post a Comment