Mahitaji
Unga wa ngano
Maji masafi
Chumvi
Mafuta ya kupikia
Hiliki
Maandalizi
- Weka unga wa ngano na hiliki kwenye bakuri
- Weka maji masafi kidogo kidogo huku ukichanganya mpaka utakapoona unga wako unakandika vizuri
- Endelea kukanda unga wako mpaka utakapo acha kunatanata mikononi
- Kisha tengeneza viduara vidogo kama ngumi
- Chukua kibao cha kusukumia sukuma iwe duara kisha chota mafuta kwa kijiko cha chakula kidogo na paka kwenye hiyo chapati
- Baada ya hapoizungushe chapatti kama unaifunga au kuikunja kuwa duara tena
- Fanya hivyo kwa maduara yote
- Kisha weka unga kidogo kwenye kibao cha kusukumia na chukua duara moja na uanze kusukuma kwa kutengeneza duara
- Bandika chombo cha kukaangia kisha weka chapati yako baada ya chombo kupata moto
- Ikiiva upande mmoja igeuze upande wa pili bila kuweka mafuta.
- Ikiwa imeiva kote sasa weka mafuta ili iive vizuri.
- Fanya hivyo kwa zote na chapati zitakuwa tayari kwa kuliwa.
No comments:
Post a Comment