Mahitaji
Maziwa
Unga wa lishe
Sukari
Maandalizi
- Bandika sufuria yenye maziwa kiasi jikoni
- Kisha korogea unga wa lishe kidogo
- Endelea kukorogea mpaka utakapoanza kutokota
- Baada ya kutokota sana unaangalia kama ni mzito sana unaweza kuongeza maziwa na kama ni mwepesi unaweza kuchukua maziwa na unga pembeni na kukoroga pembeni kisha kumimina taratibu huku ukiwa unakorogea.
- Baada ya hapo ukisha tokota utaangalia kama umeiva kwa kuona sio mwepesi sana wala mzito sana
- Weka sukari baada ya uji kutokota.
- Subiri dakika chache sukari itokote ili ikolee vizuri kwenye uji
- Ipua na weka kwenye bakuri au chupa ya chai kwaajili ya kuandaa mezani kwa kuliwa.
No comments:
Post a Comment