Pages

Tuesday, 18 April 2017

PILAU


Pilau ni chakula kinacholiwa na wengi katika hafla mbalimbali na watu wengi husema sherehe bila pilau basi bado haijakamilika. Tuangalie pishi la pilau
            Mahitaji
Kitunguu maji
Vitunguu swaumu
Viungo vya pilau
Chumvi
Maji
Mafuta ya kupikia
Mchele

















           Maandalizi
  1. Unakaanga kitunguu maji na kitunguu swaumu  kwa mafuta kiasi yani kama kijiko kimoja cha kulia chakula
  2. Unaweka viungo vya pilau  vilivyosagwa kisha unavikaanga
  3. Weka mchele kisha geuza na weka maji kiasi  kulingana na mchele kisha weka chumvi kiasi
  4. Acha vitokote ili viweze kuiva vizuri
  5. Maji yakikauka angalia kama pilau limeiva vizuri kisha palia juu na chini kama unapikia mkaa na kama ni gesi angalia kama umeiva vzr na upunguze moto kabisa ili ukauke vizuri.
  6. Pilau lako litakuwa tayari baada ya kuiva vizuri.

KACHUMBARI

Kachumbali hupenda kuliwa na vyakula mbalimbali kwani huleta hamu ya kula chakula na hivyo kufanya mtu kuvutiwa na chakula.
              Mahitaji
Vitunguu maji 3
Hoho 1
Karoti 1
Nyanya 4
Chumvi
Ndimu 1
Tango 1

Maandalizi
  1. Osha viungo vyote kwa chumvi kiasi na maji ya uvuguvugu
  2. Katakata nyanya kwa namna ya duara kisha weka kwenye bakuri
  3. Kisha katakata karoti na tango duara
  4. Katakata hoho kwa wima yani ziwe kama namba moja kisha weka vyote kwenye bakuri ya nyanya
  5. Katakata vitunguu maji  weka kwenye bakuri tofauti kisha weka chumvi na vifinyange kwa chumvi ilikupunguza  makali ya vitunguu maji.
  6. Kisha osha vizuri kwa maji na kamua  ili kuhakikisha chumvi haipo kwenye vitunguu tena na maji hayapo
  7. Weka vitunguu kwenye bakuri yenye vitu vyote na kisha changanya vizuri kwa kutumia kijiko.
  8. Baada ya hapo weka chumvi kidogo na maji ya ndimu ambayo umeikamua
  9. Kisha changanya na kachumbari yako itakuwa tayari kuliwa                                     

Thursday, 13 April 2017

NDIZI MZUZU NA NYAMA YA KUKU

Ndizi mzuzu ni aina ya ndizi ambayo ni tamu sana hasa unapoipika vizuri .Leo tutazipika bila mafuta.

     Mahitaji
Ndizi mzuzu
Chumvi
Nazi
Binzari nyembamba
Kuku robo
Nyanya
Kitunguu maji
Kitunguu swaumu
Karoti
Hoho










Maandalizi
  1. Menya ndizi zako vizuri kisha weka kwenye maji ili zisiwe nyeusi.
  2. Weka ndizi zako kwenye sufuria safi kisha weka Nazi tui la pili jepesi ili zichemke kwa Nazi
  3. Kisha weka vitunguu swaumu na vitunguu maji
  4. Baada ya hapo weka nyanya, karoti, na hoho
  5. Kisha weka vipande vya kuku vilivyochemshwa vizuri ilivichemke tena na ndizi 
  6. Weka tui la pili zito la Nazi na koroga mpaka lichemke vizuri
  7. Weka chumvi na binzari nyembamba kidogo sana
  8. Ipua ndizi kwaajili ya kuliwa

MAHARAGE

Maharage ni mboga ambayo huliwa na familia nyingi nchini na yanaasili ya kuwa na protein nyingi hivyo husaidia katika urutubishaji mwili wa binadamu.

Mahitaji
Maharage
Vitunguu swaumu
Vitunguu maji
Karoti
Pilipili hoho
Chumvi
Nazi
Tangawizi








Maandalizi
  1. Chambua, osha na kisha chemsha maharage yako mpaka yaive vizuri hakikisha maji ya kwanza yanakuwa mengi ili maharage yasiungue.
  2. Yakishaiva ipua na chukua sufuria ya kukaangia na weka mafuta kidogo sana
  3. Weka kitunguu maji ulichokatakata na baadae kitunguu swaumu na tangawizi
  4. Weka maharage na kisha weka nazi tui la pili na koroga mpaka lichemke vizuri
  5. Kisha weka tui la kwanza  zito nalo lichemke vizuri ndo uache kukoroga
  6. Weka hoho na karoti baada ya tui la kwanza zito  kuchemka na uache vichemke kidogo kisha weka na chumvi kidogo kutokana na wingi wa maharage yako.
  7. Baada ya hapo maharage yako yatakuwa yameiva vizuri sana.

Wednesday, 12 April 2017

CHAPATI ZA KUKANDA

Chapati za kukanda ni moja ya kitafunwa kinachotumika wakati wote na wakati mwingine hupendwa kuliwa ni wakati wa mfungo wa kwaresma au ramadhani.


    Mahitaji
Unga wa ngano
Maji masafi
Chumvi
Mafuta ya kupikia
Hiliki


Maandalizi

  1. Weka unga wa ngano na hiliki  kwenye bakuri
  2. Weka maji masafi kidogo kidogo huku ukichanganya mpaka utakapoona unga wako unakandika vizuri
  3. Endelea kukanda unga wako mpaka utakapo acha kunatanata mikononi
  4. Kisha tengeneza  viduara vidogo kama ngumi
  5. Chukua kibao cha kusukumia  sukuma iwe duara kisha chota mafuta kwa kijiko cha chakula kidogo na paka kwenye hiyo chapati
  6. Baada ya hapoizungushe chapatti kama unaifunga au kuikunja kuwa duara tena
  7. Fanya hivyo kwa maduara yote
  8. Kisha weka unga kidogo kwenye kibao cha kusukumia na chukua duara moja na uanze kusukuma kwa kutengeneza duara
  9. Bandika chombo cha kukaangia kisha weka chapati yako baada ya chombo kupata moto
  10. Ikiiva upande mmoja igeuze upande wa pili bila kuweka mafuta.
  11. Ikiwa imeiva kote sasa weka mafuta ili iive vizuri.
  12. Fanya hivyo kwa zote na chapati zitakuwa tayari kwa kuliwa.

UJI WA LISHE

Uji wa lishe ni kinywaji na chakula ambacho husaidia sana watu wengi kupata vitamin ambavyo vinasaidia mwili kupambana na magonjwa mbalimbali na husaidia katika ukuwaji wa watoto wadogo.
       Mahitaji
Maziwa
Unga wa lishe
Sukari












Maandalizi


  1. Bandika sufuria yenye maziwa kiasi jikoni
  2. Kisha korogea unga wa lishe kidogo
  3. Endelea kukorogea mpaka utakapoanza kutokota
  4. Baada ya kutokota sana unaangalia kama ni mzito sana unaweza kuongeza maziwa na kama ni mwepesi unaweza kuchukua maziwa na unga pembeni na kukoroga pembeni kisha kumimina taratibu huku ukiwa unakorogea.
  5. Baada ya hapo ukisha tokota utaangalia kama umeiva kwa kuona sio mwepesi sana wala mzito sana
  6. Weka sukari baada ya uji kutokota.
  7. Subiri dakika chache sukari itokote ili ikolee vizuri kwenye uji
  8. Ipua na weka kwenye bakuri au chupa ya chai kwaajili ya kuandaa mezani kwa kuliwa.

Tuesday, 11 April 2017

SAMAKI WA KUKAANGA

Samaki wa kukaanga ni mtamu sana hasa akiliwa na kachumbari na ugali kwani ni kitoweo kizuri sana na samaki wanapatikana sana katika maeneo yenye bahari au mto pia wengine hufuga samaki ilikuuza kama biashara kwani ni kitoweo kinachopendwa.
                                                                                         Mahitaji
Samaki
Vitunguu swaumu
Tangawizi
Ndimu


Matayarisho                 


  1. Osha samaki wako vizuri ukiwa umewatoa magamba yote
  2. Weka tangawizi,vitunguu swaumu na ndimu kisha subiri dakika chache
  3. Weka mafuta kwenye  kwenye chombo cha kukaangia  yakipata moto weka samaki
  4. Kisha acha waive upande mmoja kisha geuza upande mwengine  
  5. Kisha chuja katika chujio na weka kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

TAMBI

Tambi ni chakula kitamu sana ambacho kinaweza kuliwa wakati wowowte yani wakati wa asubuhi,mchana au jioni.Chakula hiki ni rahisi kupika kwa watu wengi hasa kwa watu ambao hawajaoa au kuolewa.
Mahitaji
Tambi
Sukari
Mafuta ya kupikia
Maji
Hiliki







Matayarisho

  1. Weka tambi katika sufuria ya saizi ya kati na kama tambi ni ndefu unaweza ukazikata mara tatu au mbili ili ziendelee kuwa ndefu kidogo.
  2. Weka maji katika sufuria yenye tambi kisha bandika jikoni zichemke kwa dakika 10 mpaka 15 huku ukihakikisha haziivi sana
  3. Kisha ipua chuja kwenye chujio toa maji yote
  4. Weka mafuta kwenye sufuria 
  5. Weka tambi kisha weka sukari na hiliki
  6. Endelea kugeuza na kisha  ipua.
  7. Tambi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa zikiwa nzuri za kuvutia.