Pages

Wednesday, 3 May 2017

CHAPATI ZA MAJI

Chapati za maji ni kitafuno kizuri sana kinacholiwa  na mtu yeyote kwani zinaasili ya ulaini na ni tamu sana.

  Mahitaji
Unga wa ngano1/4
Maji
Mayai 2
Sukari
Pilipili hoho
Kitunguu maji
Mafuta ya kupikia












Maandalizi
  1. Weka unga wa ngano kwenye bakuri kisha weka maji kidogo kidogo
  2. Koroga mpaka  utengeneze ujiuji mzito na baadae hakikisha hauwi mzito sana wala mwepesi sana uwe kawaida.
  3. Weka mayai yako ,hoho na kitunguu maji kisha changanya vizuri
  4. Weka sukari kidogo kulingana na kiasi cha unga na maji unaweza weka vijiko vitatu vya kulia chakula .
  5. Weka mafuta ya kula kidogo kwenye chombo cha kukaangia au flampeni
  6. Yakipata moto chota unga wako kwa kikonbe na mimina kiasi kwenye flampeni hakikisha unachota kiasi na haujazi kikombe chako kama ni cha chai.
  7. Chapata haitakiwi iwe nene sana na hivyo usimimine nyingi kujaza chombo chako weka kiasi kwa kuzungusha duara ili itokee vizuri.
  8. Ikiiva geuza upande wa pili na weka mafuta tena kidogo ili isishike chini ya chombo chako .
  9. Ikiiva unaweza kuianda na kuweza kula.



Tuesday, 2 May 2017

KABICHI

Kabichi ni mboga ya pekee ambayo unaweza kuila mbichi yani kama kachumbari au kuila ikiwa imepikwa. Kabichi huweza kuliwa na watu wote hata wale wanaotaka kupungua mwili ni nzuri sana.
    Mahitaji
Kabichi
Karoti
Kitunguu maji
Kitunguu swaumu
Hoho
Mafuta ya kupikia
Chumvi













                          




 Maandalizi

Weka mafuta kwenye sufuria kisha weka kitunguu maji baada ya mafuta kuchemka vizuri
Kisha weka kitunguu swaumu na baadae  weka karoti na hoho
Kisha weka kabichi na geuza na changanya vizuri
Hakikisha Kabichi isiive sana kisha weka chumvi kidogo.
Ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa.

MTORI

Mtori ni moja ya chakula kitamu sana ambacho huliwa na watu wa makabila mbalimbali lakini nchi Tanzania ni chakula maarufu sana kwa wachaga.Chakula hiki kinaliwa na watu mbalimbali kama kifungua kinywa na kwa wengine chakula kikuu kikiambatana na vitafunwa kama maandazi au chapatti.Wagonjwa au mama aliyejifungua na hata mtoto huweza kumfaa sana kwani kinaasili ya ujiuji.
          Mahitaji
Ndizi za matoke
Chumvi
Supu ya nyama ya ng`ombe
Karoti
Brenda
Pilipili
Ndimu


  







    Maandalizi
Menya na chemsha ndizi zako vizuri kisha zichemshe mpaka zilainike vizuri ila zisiwe ujiuji.
Mwaga maji yaliyobaki kwenye sufuria ya kuchemshia kisha weka ndizi kwenye brenda
Saga ndizi pamoja na karoti kwenye brenda huku ukiongeza supu ya nyama kidogo kidogo kwasababu unatakiwa utoke uji mzito.
Weka chumvi kidogo
Hakikisha unaweka supu bila nyama.
Weka kwenye bakuri  kisha weka nyama kama mbili au nne za supu
Weka pilipili na ndimu pembeni ya sahani kisha unaweza kula kwani utakuwa tayari.

Tuesday, 18 April 2017

PILAU


Pilau ni chakula kinacholiwa na wengi katika hafla mbalimbali na watu wengi husema sherehe bila pilau basi bado haijakamilika. Tuangalie pishi la pilau
            Mahitaji
Kitunguu maji
Vitunguu swaumu
Viungo vya pilau
Chumvi
Maji
Mafuta ya kupikia
Mchele

















           Maandalizi
  1. Unakaanga kitunguu maji na kitunguu swaumu  kwa mafuta kiasi yani kama kijiko kimoja cha kulia chakula
  2. Unaweka viungo vya pilau  vilivyosagwa kisha unavikaanga
  3. Weka mchele kisha geuza na weka maji kiasi  kulingana na mchele kisha weka chumvi kiasi
  4. Acha vitokote ili viweze kuiva vizuri
  5. Maji yakikauka angalia kama pilau limeiva vizuri kisha palia juu na chini kama unapikia mkaa na kama ni gesi angalia kama umeiva vzr na upunguze moto kabisa ili ukauke vizuri.
  6. Pilau lako litakuwa tayari baada ya kuiva vizuri.

KACHUMBARI

Kachumbali hupenda kuliwa na vyakula mbalimbali kwani huleta hamu ya kula chakula na hivyo kufanya mtu kuvutiwa na chakula.
              Mahitaji
Vitunguu maji 3
Hoho 1
Karoti 1
Nyanya 4
Chumvi
Ndimu 1
Tango 1

Maandalizi
  1. Osha viungo vyote kwa chumvi kiasi na maji ya uvuguvugu
  2. Katakata nyanya kwa namna ya duara kisha weka kwenye bakuri
  3. Kisha katakata karoti na tango duara
  4. Katakata hoho kwa wima yani ziwe kama namba moja kisha weka vyote kwenye bakuri ya nyanya
  5. Katakata vitunguu maji  weka kwenye bakuri tofauti kisha weka chumvi na vifinyange kwa chumvi ilikupunguza  makali ya vitunguu maji.
  6. Kisha osha vizuri kwa maji na kamua  ili kuhakikisha chumvi haipo kwenye vitunguu tena na maji hayapo
  7. Weka vitunguu kwenye bakuri yenye vitu vyote na kisha changanya vizuri kwa kutumia kijiko.
  8. Baada ya hapo weka chumvi kidogo na maji ya ndimu ambayo umeikamua
  9. Kisha changanya na kachumbari yako itakuwa tayari kuliwa                                     

Thursday, 13 April 2017

NDIZI MZUZU NA NYAMA YA KUKU

Ndizi mzuzu ni aina ya ndizi ambayo ni tamu sana hasa unapoipika vizuri .Leo tutazipika bila mafuta.

     Mahitaji
Ndizi mzuzu
Chumvi
Nazi
Binzari nyembamba
Kuku robo
Nyanya
Kitunguu maji
Kitunguu swaumu
Karoti
Hoho










Maandalizi
  1. Menya ndizi zako vizuri kisha weka kwenye maji ili zisiwe nyeusi.
  2. Weka ndizi zako kwenye sufuria safi kisha weka Nazi tui la pili jepesi ili zichemke kwa Nazi
  3. Kisha weka vitunguu swaumu na vitunguu maji
  4. Baada ya hapo weka nyanya, karoti, na hoho
  5. Kisha weka vipande vya kuku vilivyochemshwa vizuri ilivichemke tena na ndizi 
  6. Weka tui la pili zito la Nazi na koroga mpaka lichemke vizuri
  7. Weka chumvi na binzari nyembamba kidogo sana
  8. Ipua ndizi kwaajili ya kuliwa

MAHARAGE

Maharage ni mboga ambayo huliwa na familia nyingi nchini na yanaasili ya kuwa na protein nyingi hivyo husaidia katika urutubishaji mwili wa binadamu.

Mahitaji
Maharage
Vitunguu swaumu
Vitunguu maji
Karoti
Pilipili hoho
Chumvi
Nazi
Tangawizi








Maandalizi
  1. Chambua, osha na kisha chemsha maharage yako mpaka yaive vizuri hakikisha maji ya kwanza yanakuwa mengi ili maharage yasiungue.
  2. Yakishaiva ipua na chukua sufuria ya kukaangia na weka mafuta kidogo sana
  3. Weka kitunguu maji ulichokatakata na baadae kitunguu swaumu na tangawizi
  4. Weka maharage na kisha weka nazi tui la pili na koroga mpaka lichemke vizuri
  5. Kisha weka tui la kwanza  zito nalo lichemke vizuri ndo uache kukoroga
  6. Weka hoho na karoti baada ya tui la kwanza zito  kuchemka na uache vichemke kidogo kisha weka na chumvi kidogo kutokana na wingi wa maharage yako.
  7. Baada ya hapo maharage yako yatakuwa yameiva vizuri sana.