Mahitaji
Unga wa ngano1/4
Maji
Mayai 2
Sukari
Pilipili hoho
Kitunguu maji
Mafuta ya kupikia
Maandalizi
- Weka unga wa ngano kwenye bakuri kisha weka maji kidogo kidogo
- Koroga mpaka utengeneze ujiuji mzito na baadae hakikisha hauwi mzito sana wala mwepesi sana uwe kawaida.
- Weka mayai yako ,hoho na kitunguu maji kisha changanya vizuri
- Weka sukari kidogo kulingana na kiasi cha unga na maji unaweza weka vijiko vitatu vya kulia chakula .
- Weka mafuta ya kula kidogo kwenye chombo cha kukaangia au flampeni
- Yakipata moto chota unga wako kwa kikonbe na mimina kiasi kwenye flampeni hakikisha unachota kiasi na haujazi kikombe chako kama ni cha chai.
- Chapata haitakiwi iwe nene sana na hivyo usimimine nyingi kujaza chombo chako weka kiasi kwa kuzungusha duara ili itokee vizuri.
- Ikiiva geuza upande wa pili na weka mafuta tena kidogo ili isishike chini ya chombo chako .
- Ikiiva unaweza kuianda na kuweza kula.
No comments:
Post a Comment