Kabichi ni mboga ya pekee ambayo unaweza kuila mbichi yani kama kachumbari au kuila ikiwa imepikwa. Kabichi huweza kuliwa na watu wote hata wale wanaotaka kupungua mwili ni nzuri sana.
Mahitaji
Kabichi
Karoti
Kitunguu maji
Kitunguu swaumu
Hoho
Mafuta ya kupikia
Chumvi
Maandalizi
Weka mafuta kwenye sufuria kisha weka kitunguu maji baada ya mafuta kuchemka vizuri
Kisha weka kitunguu swaumu na baadae weka karoti na hoho
Kisha weka kabichi na geuza na changanya vizuri
Hakikisha Kabichi isiive sana kisha weka chumvi kidogo.
Ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa.
No comments:
Post a Comment