Mahitaji
Unga wa ngano 1/2
Mafuta ya kupikia1/2 kikombe
Hamira kijiko 1
Chumvi 1/4 kijiko kidogo
Ufuta
Maji masafi
Yai
Matayarisho
- Weka unga wa ngano kwenye bakuri
- Changanya viungo vikavu kama hamira na chumvi.
- weka mafuta kidogo kama robo ya kikombe ulichonacho
- Weka maji masafi kidogo kidogo huku ukichanganya mpaka ukandike vizuri usinate mkononi
- Acha uumuke
- Gawa katika matonge madogo kama ngumi
- Weka kwenye sufuria ambayo utaweka mafuta kidogo chini, kisha kuweka matonge
- Kisha paka yai juu ya matonge yako na nyunyuzia ufuta kidogo kwa kila tonge.
- Kisha weka kwenye oven au pikia mkaa kwa kuweka moto kidogo juu na chini kisha acha kwa dakika 30 na angalia mpaka utakapoona imeiva vizuri na kuwa kahawia ndipo utajua imeiva vizuri.
Mikate yetu haina sukari inatiwa chumvi kidogo sana kutokana na mahitaji ya mtu.Kwa mtu mwenye pressure inamfaa kwani haitiwi chumvi nyingi wala mafuta mengi na unapopika mwenyewe unakadilia kiwango sahihi cha chumvi ndio maana ni muhimu kupika mwenyewe.
ReplyDelete