Pages

Wednesday, 22 March 2017

MAANDAZI


Maandazi ni moja ya kitafunwa kizuri ambacho hupendwa na watu wengi karibuni ukanda wote wa Africa ya Mashariki.Wengine hupenda kula na chai ya rangi,chai ya maziwa,soda au kula maandazi kwa mchuzi au maharage.




       Mahitaji
Unga wa ngano kilo 1
Hiliki 1/4 kijiko
Sukari
Mafuta ya kupikia
Hamira
Baking powder 1/2 kijiko kidogo
Maji masafi











Maandalizi

  1. Weka ungawa ngano kwenye bakuri 
  2. Changanya vitu vyote vikavu kama sukari, hiliki, hamira na baking powder
  3. Weka mafuta kidogo robo kikombe cha chai kisha changanya.
  4. Weka maji kidogo kidogo kisha kanda unga wako mpaka ulainike na usinate mkononi .kisha wacha uumuke kidogo kama dakika 5 au 10.
  5. Baada ya hapo tengeneza duara kisha kata upendavyo kama duara kwa kutumia glasi  au pembe nne kwa kutumia kisu.
  6. Anza kuyapika au kuyachoma kwenye mafuta  yako yaliyochemka vizuri 
  7. Kisha ipua yakiwa yamepata rangi ya kahawia kama kwenye picha inavyoonyesha. 
          Maandazi yako yatakuwa tayari kwa kuliwa.




KUKU WA KUKAANGA

Kuku ni nyama nzuri ambayo ukiipika sawa sawa na viungo mbalimali basi utamu wake hauishi mdomoni mwa watu.
          Mahitaji
Kuku mzima
Vitunguu swaumu 2
Ndimu 2
Tangawizi 1
Mafuta ya kupikia
Chumvi 1/4 kijiko kidogo







Maandalizi

  1. Mkatekate  kuku katika vipande vidogo unavyotaka.
  2. Weka vitunguu swaumu na tangawizi ulivyomenya na kuvitwanga vizuri
  3. Weka ndimu na chumvi kisha acha kwa muda wa dakika 10 ili viungo vikolee kwenye kuku.
  4. Bandika mafuta jikoni na yakipata moto weka kuku wako jikoni.
  5. Wageuze na kuona wanarangi ya kahawiha kisha waipue baada ya kuiva na wachuje mafuta kwenye chujio.
  6. Kuku wako watakuwa tayari kuliwa baada ya kutoka mafuta na unaweza ukala kwa ugali au kwa chakula chochote.














SKONSI/MKATE

Skonsi ni aina ya mkate ambao unatumiwa na watu kwaajili ya kutumia kama kitafunwa.


Mahitaji
Unga wa ngano 1/2
Mafuta ya kupikia1/2 kikombe
Hamira    kijiko 1
Chumvi 1/4 kijiko kidogo
Ufuta
Maji masafi
Yai



Matayarisho

  1. Weka unga wa ngano kwenye bakuri 
  2. Changanya viungo vikavu kama hamira na chumvi.
  3. weka mafuta kidogo kama robo ya kikombe ulichonacho
  4. Weka maji masafi  kidogo kidogo huku ukichanganya mpaka ukandike vizuri usinate mkononi
  5. Acha uumuke 
  6. Gawa katika matonge madogo kama ngumi 
  7. Weka kwenye sufuria ambayo utaweka mafuta kidogo chini, kisha kuweka matonge
  8.  Kisha paka yai juu ya matonge yako na nyunyuzia ufuta kidogo kwa kila tonge.
  9. Kisha weka kwenye oven au pikia mkaa kwa kuweka moto kidogo juu na chini kisha acha kwa dakika 30 na angalia mpaka utakapoona imeiva vizuri na kuwa kahawia ndipo utajua imeiva vizuri.

UGALI

Ugali ni chakula kikuu katika familia nyingi nchini Tanzania. Chakula kinaliwa na mboga mbalimbali na hivyo kukifanya chakula hiki kuwa maarufu sana. 

  Mahitaji
Unga wa  sembe 1/4
Maji 











Maandalizi
  1. Weka maji kiasi kwenye sufuria ambayo ni saizi ya kati
  2. Korogea unga kidogo kabla maji hayajachemka sana 
  3. Endelea kukoroga mpaka uwe uji mzito kidogo unaochemka kisha acha uji uchemke kwa dakika chache.
  4. Baada ya kuchemka uji anza kuweka unga kidogo kidogo kisha songa ugali wako mpaka utakapo iva vizuri.
  5. Baada ya kuiva utaona umeanza kuweka ukoko kidogo kwenye sufuria ma hivyo utaipua ukiwa umeiva vizuri na utakuwa tayari kwa kuliwa.