Pages

Wednesday, 3 May 2017

CHAPATI ZA MAJI

Chapati za maji ni kitafuno kizuri sana kinacholiwa  na mtu yeyote kwani zinaasili ya ulaini na ni tamu sana.

  Mahitaji
Unga wa ngano1/4
Maji
Mayai 2
Sukari
Pilipili hoho
Kitunguu maji
Mafuta ya kupikia












Maandalizi
  1. Weka unga wa ngano kwenye bakuri kisha weka maji kidogo kidogo
  2. Koroga mpaka  utengeneze ujiuji mzito na baadae hakikisha hauwi mzito sana wala mwepesi sana uwe kawaida.
  3. Weka mayai yako ,hoho na kitunguu maji kisha changanya vizuri
  4. Weka sukari kidogo kulingana na kiasi cha unga na maji unaweza weka vijiko vitatu vya kulia chakula .
  5. Weka mafuta ya kula kidogo kwenye chombo cha kukaangia au flampeni
  6. Yakipata moto chota unga wako kwa kikonbe na mimina kiasi kwenye flampeni hakikisha unachota kiasi na haujazi kikombe chako kama ni cha chai.
  7. Chapata haitakiwi iwe nene sana na hivyo usimimine nyingi kujaza chombo chako weka kiasi kwa kuzungusha duara ili itokee vizuri.
  8. Ikiiva geuza upande wa pili na weka mafuta tena kidogo ili isishike chini ya chombo chako .
  9. Ikiiva unaweza kuianda na kuweza kula.



Tuesday, 2 May 2017

KABICHI

Kabichi ni mboga ya pekee ambayo unaweza kuila mbichi yani kama kachumbari au kuila ikiwa imepikwa. Kabichi huweza kuliwa na watu wote hata wale wanaotaka kupungua mwili ni nzuri sana.
    Mahitaji
Kabichi
Karoti
Kitunguu maji
Kitunguu swaumu
Hoho
Mafuta ya kupikia
Chumvi













                          




 Maandalizi

Weka mafuta kwenye sufuria kisha weka kitunguu maji baada ya mafuta kuchemka vizuri
Kisha weka kitunguu swaumu na baadae  weka karoti na hoho
Kisha weka kabichi na geuza na changanya vizuri
Hakikisha Kabichi isiive sana kisha weka chumvi kidogo.
Ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa.

MTORI

Mtori ni moja ya chakula kitamu sana ambacho huliwa na watu wa makabila mbalimbali lakini nchi Tanzania ni chakula maarufu sana kwa wachaga.Chakula hiki kinaliwa na watu mbalimbali kama kifungua kinywa na kwa wengine chakula kikuu kikiambatana na vitafunwa kama maandazi au chapatti.Wagonjwa au mama aliyejifungua na hata mtoto huweza kumfaa sana kwani kinaasili ya ujiuji.
          Mahitaji
Ndizi za matoke
Chumvi
Supu ya nyama ya ng`ombe
Karoti
Brenda
Pilipili
Ndimu


  







    Maandalizi
Menya na chemsha ndizi zako vizuri kisha zichemshe mpaka zilainike vizuri ila zisiwe ujiuji.
Mwaga maji yaliyobaki kwenye sufuria ya kuchemshia kisha weka ndizi kwenye brenda
Saga ndizi pamoja na karoti kwenye brenda huku ukiongeza supu ya nyama kidogo kidogo kwasababu unatakiwa utoke uji mzito.
Weka chumvi kidogo
Hakikisha unaweka supu bila nyama.
Weka kwenye bakuri  kisha weka nyama kama mbili au nne za supu
Weka pilipili na ndimu pembeni ya sahani kisha unaweza kula kwani utakuwa tayari.